Ruka hadi Yaliyomo

Mamlaka na kazi za kaunti ni—

  1. Kilimo, pamoja na–
    (a) Kilimo cha mimea na wanyama;
    (b) Viwanja vya kuuzia wanyama;
    (c) Vichinjio vya kauni;
    (d) Udhibiti wa magonjwa ya mimea na wanyama; na
    (e) Uvuvi.
  2. Huduma za afya za kaunti pamoja na, hasa—
    (a) Vituo vya afya vya kaunti na maduka ya dawa;
    (b) huduma za magari ya wagonjwa;
    (c) Kuimarisha afya ya kimsingi;
    (d) Kutoa leseni na kusimamia shughulia za kuuza vyakula kwa umma;
    (e) Huduma za utabibu wa wanyama (isipokuwa usimamizi wa taaluma hii);
    (f) Makaburi, kumbi za matanga na tanuu za kuchomea maiti; na
    (g) Uondoaji taka, maeneo ya kutupa taka na utupaji taka.
  3. Kudhibiti uchafuzi wa hewa, uchafuzi wa mazingira kupitia kelele, na usumbufu mwingine kwa umma na utangazaji nje ya makazi.
  4. Shughuli za kitamaduni, burudani za umma na huduma za kufurahisha umma pamoja na—
    (a) Kucheza dau, kasino na njia nyingine za kamari;
    (b) mashindano ya mbio;
    (c) Utaoji leseni kwa pombe;
    (d) majumba ya Sinema;
    (e) maonyesho ya video na kukodisha;
    (f) maktaba;
    (g) makavazi;
    (h) michezo na shughuli za kitamaduni na vifaa; na
    (i) bustani za kaunti, fuo na nyenzo za burudani.
  5. Uchukuzi katika kaunti, pamoja na—
    (a) barabara za kaunti;
    (b) taa za barabarani;
    (c) magari na uegeshaji;
    (d) usafiri wa barabarani kwa umma; na
    (e) vivuko na bandari, isipokuwa usimamizi wa usafiri majini wa kitaifa na kimataifa na shughuli zinazohusiana na hizo.
  6. Udhibiti na hali ya wanyama, pamoja na–
    (a) kutoa leseni kwa mbwa; na
    (b) Nyenzo za kuhifadhi, kutunza na kuzika wanyama.
  7. Ustawishaji wa biashara na usimamizi, pamoja na—
    (a) masoko;
    (b) leseni za biashara (isipokuwa udhibiti wa taaluma hizo);
    (c) usawa katika shughuli za kibiashara;
    (d) utalii wa humu nchini; na
    (e) vyama vya ushirika.
  8. Mipango na maendeleo ya kaunti, pamoja na—
    (a) takwimu;
    (b) usoroveya na uchoraji ramani;
    (c) mipaka na ujenzi wa nyua;
    (d) makazi; na
    (e) Uunganishaji na udhibiti wa nguvu za umeme na gesi.
  9. Elimu ya chekechea, elimu, vyuo vya ufundi anuwai, vituo vya utengenezaji wa vyombo vya kinyumbani na nyenzo za utunzaji wa watoto.
  10. Utekelezwaji wa sera maalum za serikali ya kitaifa kuhusu maliasili na uhifadhi wa mazingira, pamoja na—
    (a) uhifadhi wa udongo na maji; na
    (b) misitu.
  11. Huduma za kazi kwa umma katika kaunti pamoja na—
    (a) mfumo wa usimamizi wa maji ya tufani katika sehemu za majengo; na
    (b) huduma za maji na usafi.
  12. huduma za kuzima moto, na usimamizi wa majanga
  13. udhibiti wa dawa na ponografia.
  14. kuhakikisha na kusimamia ushiriki wa jamii na sehemu za mashambani katika utawala wa viwango hivyo vya mashinani na kuzisaidia jamii pamoja na maeneo hayo kujenga uwezo wa kiusimamizi ili kuwezesha matumizi ya mamlaka na majukumu na kushiriki katika utawala wa mashinani.