(1) Hakuna kodi yoyote au malipo ya leseni yanayoweza kuondolewa au kubadilishwa ila kwa mujibu wa sheria.
(2) Iwapo sheria itaruhusu kufutiliwa mbali kwa ushuru au malipo ya leseni–
- (a) rekodi ya kufutilia mbali itahifadhiwa kwa umma ambayo itaonyesha sababu za kila kufutilia mbali; na
- (b) kila kufutiliwa mbali, pamoja na sababu zake lazima zifikishwe kwa Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu.
(3) Hakuna sheria ambayo itamwondolea au kuamrisha mhudumu yeyote wa umma kutolipa kodi kwa sababu za–
- (a) mamlaka yanayoshikiliwa na afisa huyo; au
- (b) aina ya kazi anayofanya afisa huyo.