Ruka hadi Yaliyomo

(1) Mtu yeyote anayezuiliwa kisheria, awe amehukumiwa au la, ana haki zote na uhuru wa kimsingi unaoelezwa kwenye Katiba hii, isipokuwa kwa kiwango kwamba haki au uhuru huo wa kimsingi hauambatani kabisa na sababu yake ya kuwa kwenye jela.

(2) Mtu yeyote aliye kizuizini ama aliyezuiliwa ana haki ya kulalamika ili kutolewa amri ya kufikishwa mahakamani.

(3) Bunge litatunga sheria ambayo–

  • (a) itatoa kanuni za kushughulikiwa kibinadamu kwa walio kizuizini, waliokamatwa au waliofungwa jela; na
  • (b) kuzingatia sheria mwafaka za haki za binadamu za kimataifa.