(1) Iwapo Bunge moja linapitisha mswada wa kawaida kuhusu kaunti, na Bunge la pili–
- (a) likaukataa Mswada huo, basi utapelekwa kwa kamati ya upatanisho chini ya Kifungu cha 113; au
- (b) linapitisha Mswada uliorekebishwa, utarejeshwa kwa lile Bunge ulikotoka mwanzoni, ili kutathminiwa tena.
(2) Ikiwa, baada ya Bunge asili lililoleta Mswada limeushughulikia upya Mswada uliorejeshwa kwake chini ya ibara ya (1) (b), basi Bunge hilo–
- (a) litaupitisha Mswada kama ulivyorekebishwa, Spika wa Bunge hilo ataupeleka kwa Rais katika muda wa siku saba ili kuidhinishwa.
- (b) linaukataa Mswada kama ulivyorekebishwa, Mswada huo unapelekwa kwa kamati ya upatanishi chini ya Kifungu cha 113.