Ruka hadi Yaliyomo
Bajeti

Ukusanyaji wa Mapato ya Kaunti nchini Kenya

Mwaka wa Fedha wa 2020/2021

Katika mwaka wa fedha wa 2020/2021, Serikali za Kaunti zilikusanya shilingi bilioni 34.44 ambazo zinajumuisha asilimia 64.2 ya lengo la mapato ya mwaka la shilingi bilioni 53.66.

Hata hivyo, mapato haya ni pungufu yakilinganishwa na shilingi bilioni 35.77 zilizokusanywa mwaka wa 2019/2020.

Uchambuzi wa mapato ya ndani ya kaunti ya mwaka wa fedha wa 2020/2021 umeonyeshwa kwenye jedwali lililo hapa chini.

KauntiLengo la MapatoMapato HalisiAsilimia (%)
Baringo346,088,720205,203,68959.3
Bomet221,421,954183,008,30282.7
Bungoma500,000,000395,118,23879
Busia1,119,555,802322,558,22728.8
Elgeyo Marakwet69,779,55069,075,37599
Embu937,782,533375,326,29140
Garissa150,000,000103,525,79269
Homa Bay170,818,374120,412,56770.5
Isiolo113,686,33757,181,28250.3
Kajiado1,687,000,000862,288,15151.1
Kakamega1,656,000,0001,118,235,98367.5
Kericho654,058,870595,976,65391.1
Kiambu3,795,881,1932,425,245,16163.9
Kilifi1,201,166,719833,845,29269.4
Kirinyaga405,000,000346,521,59985.6
Kisii650,000,000403,001,86062
Kisumu1,579,172,106822,299,84852.1
Kitui600,000,000326,450,31154.4
Kwale365,641,316250,090,34668.4
Laikipia1,006,875,000840,396,63283.5
Lamu100,000,000108,433,650108.4
Machakos1,299,758,6301,296,364,66899.7
Makueni1,019,949,654527,527,34151.7
Mandera200,037,792143,313,89871.6
Marsabit150,000,000110,368,25373.6
Meru600,000,000435,932,40672.7
Migori285,000,000288,535,155101.2
Mombasa6,459,442,1593,314,532,17851.3
Murang'a900,000,000627,164,59869.7
Nairobi City16,209,511,1709,958,038,68161.4
Nakuru1,800,000,0001,628,821,53790.5
Nandi405,408,260261,039,02764.4
Narok1,405,874,324618,992,78344
Nyamira250,000,000162,863,88065.1
Nyandarua954,000,000408,718,25942.8
Nyeri1,000,000,000886,892,73488.7
Samburu80,312,31970,378,82787.6
Siaya420,000,000332,883,06179.3
Taita Taveta363,000,000302,005,40083.2
Tana River72,600,00083,075,805114.4
Tharaka Nithi350,000,000254,745,60272.8
Trans Nzoia493,799,500340,453,74668.9
Turkana175,000,000209,830,607119.9
Uasin Gishu991,000,0001,105,676,540111.6
Vihiga216,096,587169,109,80278.3
Wajir150,000,00073,955,72249.3
West Pokot78,052,20268,866,91088.2
Jumla53,658,771,07134,444,282,66964.2

Kutoka tarehe 1 Julai 2020 hadi 30 Juni 2021. Ripoti Asili: Ripoti ya Msimamizi wa Bajeti ya 2020/21(Kiungo cha Nje)

Uchambuzi wa ukusanyaji wa mapato ya ndani ya kaunti unaonyesha Serikali za Kaunti zifuatazo ziliweza kuzidi lengo lao la makadirio ya mapato ya mwaka–

  • Turkana kwa asilimia 119.9,
  • Tana River kwa asilimia 114.4,
  • Uasin Gishu kwa asilimia 111.6,
  • Lamu kwa asilimia 108.4, na
  • Migori kwa asilimia 101.2.

Hata hivyo, Serikali tano za Kaunti hazikufikia malengo yao ya makadirio ya mapato ya mwaka–

  • Wajir kwa asilimia 49.3,
  • Narok kwa asilimia 44,
  • Nyandarua kwa asilimia 42.8,
  • Embu kwa asilimia 40, na
  • Busia kwa asilimia 28.8.